Kwa ufupi
Katika swali hilo la nyongeza, Shangazi auliza udhibiti wa Serikali katika vyuo vinavyotoa elimu bila kufuata miongozo
Dodoma. Serikali imesema itaendelea kuvifuatilia na kuvifungia vyuo vikuu vinavyotoa elimu bila kuzingatia miongozo, kanuni na sheria zilizowekwa.
Kauli hiyo imetolewa leo Aprili 27, 2018 na Naibu Waziri wa Elimu, William Ole Nasha wakati akijibu swali la nyongeza Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Mmasi lililoulizwa kwa niaba yake na mbunge wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi.
Katika swali hilo la nyongeza, Shangazi aliuliza udhibiti wa Serikali katika vyuo vinavyotoa elimu bila kufuata miongozo.
Akijibu swali hilo Ole Nasha amesema mwaka huu Serikali imevifungia vyuo 19, kusitisha programu 75 za vyuo 19.
“ Tumekuwa tukiielekeza tume ya vyuo vikuu kudhibiti ubora wa elimu ili kuhakikisha taratibu zote zinafuatwa. Pia Serikali tumekuwa tukizingatia uhuru wa vyuo hivi lakini tumekuwa tukivifuatilia kuhakikisha kuwa utendaji wake unazingatia taratibu tulizoziweka,” amesema.
0 Comments