VYUO VIKUU VYATAKIWA KUTOA ELIMU YAKUJIAJIRI - PROF ELISANTE OLE GABRIEL







WIZARA ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imewashauri viongozi wa vyuo vikuu nchini kutoa elimu ya vitendo kwa wanafunzi badala ya kuegemea kinadharia, ili kujenga uwezo wa wahitimu kujiajiri.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Elisante ole Gabriel alisema hayo hivi karibuni mjini Morogoro wakati akifungua Mkutano mkuu wa taifa wa jumuiya ya Waadventisti Wanataaluma na Wajasiriamali wa Tanzania (ATAPE). Mkutano huo mkuu uliokuwa chini ya Mnenaji, Askofu mkuu wa kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) Jimbo kuu la kusini mwa Tanzania, Mark Malekana.
Alisema hatua hiyo itawawezesha baada ya kuhitimu elimu ya juu watakuwa na uwezo wa kuazisha vitega uchumi vya kibiashara na viwanda vya ukubwa tofauti, ambavyo vitakuwa ni chachu kwao kuwaajiri Watanzania wenzao. Hata hivyo, alisema ni vyema wasomi wanapohitimu elimu ya vyuo vikuu katika fani moja, wakajiendeleza zaidi kusomea fani nyingine ambazo zitawasaidia kupambana na kukosa ajira ama kujiajiri kulingana na mahitaji ya soko.
Katika hatua nyingine alisema, kuanzia Juni mwaka huu wizara hiyo inatarajia kuanzisha mfumo mmoja wa malipo utakaotawanya kwenye taasisi zilizopo chini yake ambazo zinahusika na michakato ya hatua mbalimbali ya kuazisha biashara ama uwekezaji wa viwanda, lengo ni kuwaondolea adha wananchi.

0 Comments