Amesema chuo hicho kitakuwa kinafanya mihadhara mbalimbali ya kitaaluma.Dodoma. Katika kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kimeandaa mdahalo wa wanataaluma huku Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki akialikuwa kuwa mgeni rasmi.
Mada kuu katika mdahalo huo utakaofanyika Mei 18, 2018 na kuwahusisha wanataaluma kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini pamoja na viongozi wastaafu na walioko madarakani ni hali ya elimu katika Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Mei 12, 2018 mjini Dodoma, Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Egid Mubofu amesema mhadhara huo ni mwanzo wa mihadhara itakayokuwa inafanyika kila mwaka chuoni hapo kwa ajili ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere.
Amesema chuo hicho kitakuwa kinafanya mihadhara mbalimbali ya kitaaluma.
Amesema Mbeki ataambatana na mkuu wa chuo hicho, Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ambaye siku za hivi karibuni alipendekeza kufanyika kwa mdahalo wa kitaifa kujadili sekta ya elimu nchini.
0 Comments