WANAFUNZI WANAOPATA MIMBA WAFICHWA- RUKWA







WANAFUNZI wanaopata ujauzito mkoani Rukwa ni zaidi ya 325 wanaotajwa na serikali.
Walimu wamesema wanafunzi wanaopata ujauzito ni wengi kuliko takwimu za Serikali mkoani.
Wamedai wazazi na walezi wamebuni mchezo mchafu wa kuficha binti zao pindi wanapopata ujauzito shuleni wakiorodheshwa watoro sugu.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mazwi, Manispaa ya Sumbawanga, Aliko Mbuba amesema wanafunzi wa kike wameanza kushiriki ngono wakiwa darasa la tatu na darasa la nne.
Amesema wanafunzi hao wakijiunga na kidato cha kwanza kutokana na ugeni wanaanza kuchangamkia ngono wafikapo kidato cha pili.
"Idadi ya wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari wanaoacha masomo kwa sababu ya ujauzito ni kubwa kuliko inayotangazwa na Serikali ya Mkoa ya wanafunzi 325, hawa ni wale waliopimwa na kubainika rasmi,’’ amesema.
Mwalimu mstaafu, Sammy Kisika amesema katika shule moja ya msingi Manispaa ya Sumbawanga nusu ya wasichana waliokuwa darasa la tatu walikuwa wameanza ngono.
Takwimu zinaonesha kuwa wanafunzi 325 wamekatiza masomo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita kutokana na ujauzito huku wa sekondari wakiwa 288 na elimu ya msingi ni 37.

0 Comments