Kama alivyowahi kunukuliwa kwamba yeye ni mpiga debe wa Tanzania ya Viwanda,jana Waziri Charles Mwijage amehamishia debe hilo kwenye shule za sekondari akisema wanafunzi waandaliwe kuchukua jukumu mbeleni kwa kuwa viwanda vinavyojengwa sasa ni vile vya kipindi cha mpito.
Akihutubia katika mahafali ya kidato cha sita kwa shule za sekondari Kaizirege na Kemebos, jana Mei 19, Waziri Mwijage,alisema viwanda vya kudumu vitajengwa na wanafunzi wanaoandaliwa vizuri katika masomo ya sayansi.
Alisema kuwa wazazi na wanafunzi wanatakiwa kusoma upepo unapoelekea ambao unawahitaji wanafunzi wa masomo ya sayansi kwa ajili ya kuchukua jukumu la.kujenga uchumi wa viwanda.
Pia aliwakumbusha wazazi na watu wenye mitaji wasikimbilie kwenye uanzishaji wa viwanda vikubwa bali waanze na viwanda vidogo na baadaye waende hatua kwa hatua hadi viwanda vikubwa.
Waziri Charles Mwijage ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kudato cha sita shule ya Sekondari Kaizirege na ya Kemebos ambapo jumla ya wanafunzi 180 wamehitimu.
0 Comments