RAIS WA ZANZIBAR AHIMIZA MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA ZA RUZUKU MASHULENI


Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein

Kwa ufupi
Fedha hizo zitatumika kuwapa wanafunzi wa shule za Sekondari za Serikali vitabu vya kuandikia, vifaa vya maabara, chaki na gharama za mitihani.

Zanzibar. Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein ameuagiza uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuhakikisha unaziingiza fedha za ruzuku katika shule za Serikali kwa wakati.

Amesema ukosefu wa ruzuku hizo isiwe sababu ya kuwafanya walimu wawe viguu na njia kwa ajili ya kufuata fedha hizo Wizarani.

Benki ya Dunia (WB) imetoa Dola 35 milioni(Sh79,807,000,000) katika utekelezaji wa sera ya elimu.

Dk. Shein ameyasema hayo leo katika sherehe ya uzinduzi wa utoaji wa ruzuku katika shule za Serikali, kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil, Kikwajuni mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.

“Nawataka watendaji wa Wizara ya Elimu kutoa ushirikiano mkubwa ili mradi huo uwe wenye mafanikio yaliyokusudiwa na ni vyema kila mmoja akatekeleza majukumu yake katika dhamana aliyonayo,” amesema

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha mradi huo unafanikiwa na kufikia malengo yaliokusudiwa yeye mwenyewe atakuwa mstari wa mbele katika kusimamia na kkutekeleza yale yote ambayo Serikali imeahidi katika mradi huo.

Fedha hizo zitatumika kwa kuwapa wanafunzi wa shule za Sekondari za Serikali vitabu vya kuandikia, vifaa vya maabara, chaki na gharama za mitihani.

Pia zitatumika kuwasaidia wanafunzi wenye uzito wa katika kuelewa na kuzizawadia shule zitakazofanya vizuri mitihani yao ya Darasa la Sita, Kidato cha Pili na Kidato cha Nne.

Dk Shein ametoa shukurani kwa Benki ya Dunia pamoja na washirika wengine kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Zanzibar katika kuimarisha sekta ya elimu.

Akieleza historia ya maendeleo ya sekta ya elimu Zanzibar, Dk. Shein amesema kuwa miongoni mwa changamoto walizopata waliosoma zamani ni pamoja na huduma hiyo pamoja na

0 Comments