Kiongozi wa HDIF, Tanzania,David McGinty akizungumza na Wahariri na Wahandishi wa Vyombo Mbalimbali vya habari pamoja na wadau wa Masuala ya Sayansi wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Ubunifu kwa Vijana inayofanyika katika Kumbi Mbalimbali za Costech Jijini Dar es Salaam chini ya ufadhili wa UKAID na HDIF.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),Dk Amos Nungu akizungumzia juu ya wiki ya Ubunifu kwa Vijana iliyoanza katika Kumbi mbali mbali za Costech ambapo wanufaika wataonesha kazi zao kwa kuwasilisha katika makongamano yatakayokuwa yanaendelea chini ya ufadhili wa HDIF kwa kushirikiana na UKAID
Naibu Kiongozi wa HDIF Tanzania, Joseph Manirakiza akieleza namna HDIF ilivyoweza kutoa ruzuku kwa wanufaika wa miradi mbalimbali ya ubunifu wakati wa ufunguzi ya wiki ya ubunifu inayoendelea katika kumbi mbalimbali za COSTECH.
Baadhi ya wanufaika wa Mradi huo wakifatilia kwa ukaribu hottuba mbalimbali zinazotolewa na wadau wa masuala ya ubunifu.
Mtaalamu wa Masula ya Mawasiliano kutoka HDIF , Hannah Mwandoloma akiw apamoja na baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari wakisikiliza mawasilisho juu ya wiki ya Ubunifu.
Wanufaika wa Wiki ya Ubunifu wakiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi wa COSTECH, HDIF na UKAID.
0 Comments