CHUO KIKUU HURIA CHATOA MSAADA HOSPITALI YA TUMBI MKOANI PWANI.




Chuo kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kimetoa msaada wa vifaa tiba mbalimbali pamoja na kuchangia damu katika Hospitali ya Tumbi mkoani Pwani.

Kwa mujibu wa mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya chuo, Kahenga Dachi,

msaada huo uliogharimu takribani shilingi millioni 10 kwa lengo la kuwasaidia akina mama na watoto.

"Ni msaada kutoka kwa baadhi ya wanafunzi na wafanyakazi wa chuo ikiwa ni utaratibu wetu wa kurudisha tulichonacho kwa jamii," alisema .

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Afya Tumbi, Dk Edward Wayi amekipongeza chuo kwa hatua hiyo na kufafanua kwamba mahitaji ya damu katika hospitali hiyo ni chupa 10 kwa siku, sawa 300 kwa mwezi.

Ameitaka jamii kuwa na mwamko wa kuchangia damu na si pale tu mtu anapokua na mgonjwa mwenye nahitaji ya damu.

Ameongeza kwamba hospitali ina utaratibu wa kutembelea taasisi mbalimbali za binafsi na serikali kuomba msaada wa kuchangia damu kutokana na hali halisi kwamba mahitaji ni endelevu.

"Tunashukuru mwamko ni mkubwa katika taasisi ambapo tunaweza kupata hata chupa 50 mpaka 60 kwa siku.

Tatizo ni kwa mtu mmoja mmoja kujitolea, ni mpaka awe na mgonjwa anayehitaji damu," alisema mkurugenzi.

Amesisitiza kwamba nahitaji ya damu ni mkubwa kwa mama na watoto pamoja na maeneo mengine yanayohusika na shughuli za upasuaji hospitalini hapo.

0 Comments