SEMINA YA TCRA KUHUSU MAHUDHUI, ARUSHA 2021.




Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA)imeendesha semina  ya siku moja,  juu ya uzalishaji wa maudhui ya ndani na uzalishaji wa uboreshaji wa maudui kwa wamiliki wa vituo vya utangazaji mtandaoni (online TV na Bloggers), katika kuzingatia kanuni, maadili, sheria za nchi pamoja na makosa ya mtandaoni.

Mhandisi Imelda Salum ni Mkuu wa Kanda ya Kaskazini (TCRA)amewataka wamiliki hao wa vyombo vya habari kuwa na ushirikiano, ubunifu ,katika utendaji kazi kwao wa kila siku, kuwa na maudhui chanya yenye mtizamo unaobeba mambo kadhaa wa kadha ,pamoja na kuongeza udadisi katika kujifunza.

 Aidha Mhandisi huyo alisema kuwa lengo kubwa la semina hiyo ni kubadilishana uzoefu, kuzijua  changamoto mbalimbali ambazo zipo na Kuona namna ambayo watazipatia ufumbuzi,pamoja na kuwakumbusha namna ya kufikiria juu ya kizazi kijacho kutokana na ukuaji wa teknolojia tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Akizungumza mwezeshaji   wa mafunzo hayo Reuben Boniface ,alisema kuwa lengo kuu la ni kuwakumbusa kutambua kuwa maudhui ya ndani kwani yana maana pana ,ikiwemo umri,jinsia,mtazamo wa kiimani,na lugha sahihi inayotumika huku akiwataka kutumia uandishi wa kuzingatia sheria za nchi bila kuleta mtafaruku.

Aidha Boniface aliwataka kufahamu kuwa wakati wa kuandaa maudhui ,watambue kwa undani juu ya yale ambayo yanayoisibu jamii, pamoja na yale ambayo yanawatia hofu,huku wakutambua kazi yao kubwa ni kuelimisha, kuhabarisha pamoja na kutoa burudani.

Akizungumza mmoja wa mshiriki wa semina hiyo Mussa Juma amesema kuwa kwa kutumia mitandao ina nafasi kubwa ya kutengeneza ajira,kupata fursa mbalimbali,kazi ama biashara kwa mtandao badala ya kukuingiza au kutengeneza maudhui ambayo hayafai kwa jamii 

Hivyo amewaasa wamiliki wa vyombo hivyo kuzingatia sheria ,kanuni na bila kusababisha uvunjifu wa amani,huku akisisitiza weledi zaidi unahitajika katika kujenga uelewa mzuri kwa jamii kwa ujumla.

  Mwezeshaji Reuben Boniface  akizungumza na  wamiliki wa  vituo vya utangazaji mtandaoni (online TV,Bloggers)  katika semina ya siku moja iliyofanyika katika hotel ya Golden Rose Jijini Arusha. Picha zote /habari na Vero Ignatus.


Baadhi ya wamiliki wa TV za mtandaoni na utangazaji maudhui mtandaoni wakifuatilia kinachoendelea katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na TCRA

Semina ikiendelea katika ukumbi wa Golden Rose Jijini Arusha.

Mkuu wa Kanda ya Kaskazini (TCRA)Mhandisi  Imelda Salum  akisikiliza mmoja wa wamiliki wa tv mtandaoni alipokuwa akichangia mada katika semina ya siku moja.

Mafunzo yakiendele ambapo Mkuu wa Kanda ya Kaskazini (TCRA )Mhandisi  Imelda Salum  kama anavyoonekana katika picha akiwasikiliza wakati wakichangia mada mbalimbali katika semina hiyo ya siku moja.

0 Comments