Ericsson Temu ni mwamuzi wa soka anayechezesha soka nchini Uingereza na kuwa ndio Mtanzania wa kwanza kuchezesha soka nchini humo.
Temu aliweka historia ya kipekee ya kuwa mwamuzi wa kwanza mtanzania kuchezesha soka nchini England, alipochezesha pambano baina ya Charlton Athletics FC dhidi ya Queens Park Rangers FC kwa wachezaji walio chini ya umri wa miaka 23.
Katika kipindi cha majuma matatu ya mwezi Desemba, Mtanzania huyu amechezesha michezo iliyohusisha Arsenal U20 dhidi ya Southend United U20, Crystal Palace U20 dhidi ya Stevenage FC U20, pia akichezesha mchezo MK Dons U20 dhidi Crystal Palace U20,
Pia Mwamuzi huyu amechezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho kwa wachezaji walio chini ya umri wa miaka 23 aliposimamia mchezo wa raudi ya tatu kati ya Herne Bay FC dhidi ya Catford Wanderers (2008)
0 Comments