Leo nitaendelea hatua ingine mbele kuibua moja ya kero Kubwa
ya wanaOlasiti na kueleza sifa za Diwani tunayemuhitaji Olasiti.
Kwa kuanza niseme wazi kuwa wananchi wa Olasiti tunakabiliwa
na tatizo la Miundomindu na Usafirishaji. Barabara zetu za mitaa Olasiti
inasikitisha kwa ujumla, nikianzia na barabara za mitaa ya Olasiti kati, Burka,
Olkereyani, Kimindoros na Oloresho,
barabara hazina mfumo uliopangika ki mipango miji, haina mifereji na baadhi
hazipitika kabisa.
Kata ya Olasiti ni
moja ya kata zilizomo ndani ya Jji la Arusha na zinaudumiwa na Halmashauri ya
Jiji la Arusha chakushangaza katika bajeti fedha zinatengwa lakini katika
ufuatiliaji na utekelezaji ndipo pana shida kubwa. Kwa mfano barabara yetu
inayoingilia kituo cha Kibo ni mbovu kwelikweli, jirani kabisa mwekezaji Kibo
pana Daraja lisilo na kiwango na shimo pembeni linaloweza leta madhara kwa
watembea kwa miguu, waendesha pikipiki hata magari, mfano mwingine ni barabara
ya Oloresho inayoelekea NJIKAKA inasikitisha kwelikweli, barabara za mitaa ya
burka, olkereyani na kipindi tukiendeacho cha Mvua baadhi hazitapitika kabisa.
Usafirishaji ni tatizo Sugu linalotukabili Wananchi wa
Olasiti, kukosekana kwa usafiri wa magari madogo ya Abiria (Hiace) inasababisha
adha kubwa, garama kubwa ya usafiri, mfano ukitaka kwenda kununua mbogamboga
soko la mbauda au soko la kilombero unatakiwa uwe na nauli ya shilingi elfu
tatu, yaani elfu moja ya pikipiki ya kutoka kwako hadi barabara ya lami alafu
mia nne ya hiace ya kwenda na kutoka sokoni. Hali hii haivumiliki kabisa
kwasababu Sumatra wametoa vibali vya usafirishaji kwa wamiliki wa Hiace
ziendazo Olasiti (Stand Olasiti)
chakushangaza ni kuona magari yao
yakielekea kwa Mrombo.
Maswali ya Kujiuliza.
Je Sumatra Arusha mnayajua haya na kuyafumbia macho? Wamiliki
wa Hiace kwanini mnafanyabiashara kunyume cha Vibali? Madereva kwanini
mnaingilia ruti zisizozenu? Wananchi kwanini mnakubali kupanda hiace imeandikwa
Standi hadi Olasiti ni mnakubali dhuluma hii?
SIFA ZA DIWANI
Kwa leo nitataja
moja, nayo kama Kiongozi wa Wananchi anapaswa
kujua TATIZO na kuchukua HATUA ya kupata UFUMBUZI wa tatizo.
Tunaamini huu ni muda muafaka wa waliopewa dhamana ya
kututumikia wananchi wa Olasiti
watatekeleza wajibu kwa mujibu wa majukumu yao, vinginevyo Wananchi wataamua kuchagua
Viongozi wengine watakaoweza KUWASIKILIZA, KUWAHESHIMU, KUWAPENDA, KUWAJALI
NA KUWATUMIKIA kwa kuwezesha barabara zetu zote kuwa za viwango bora na kupitika wakati wote.
USHAURI WA KWELI
NI WANANCHI WA OLASITI CHAGUENI CHADEMA KATIKA
UCHAGUZI UJAO WA SERIKALI ZA MITAA NA UDIWANI KWA MAENDELEO NA DEMOKRASIA YA
KWELI.
“CHADEMA NDIO TUMAINI PEKEE LA WANAOLASITI”
Makala hii imesheheni ukweli na ushaidi si porojo pekee
0 Comments