TATIZO LA KIWANDA CHA (A TO Z) KUCHAFUA MAZINGIRA.
OLASITI
Kweli kuna Janga linalosabaishwa na
Mwekezaji wa Kiwanda cha (A to Z) kwa kuelekeza mfumo wa maji taka wa
kiwanda kwenye moja ya Mto unaopatikana Kata ya Olasiti, Mtaa wa
Oloresho, Mto Oloresho.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Oloresho, Ndugu.
Eliakimu Olodi akieleza Sakata lote alianza
“ Mimi nilipokea simu toka kwa Balozi nikiwa kanisani akinijulisha wananchi wameitisha kikao cha dharura na wananihitaji kwa haraka, ikanibidi nitoke kanisani nije kujua dhumuni la kikao, nilipofika nikawakuta wanachi wakiwa na Hasira sana kutokana na kiwanda cha (A to Z) kutiririsha maji machafu, yenye rangi ya sumu kwenye chanzo cha maji cha Mto Oloresho na wananchi walipanga kuandamana”
“Basi nikawaomba wananchi, tusichukua
hatua ya haraka kabla yakuwa uthibitisho na uhakika wa jambo
tulifanyalo, kwahiyo baada ya malumbano ya hoja ya muda mrfu
tuliazimia, tukakague mfereji na madhara yaliyosababishwa na maji
hayo, ndio unatuona tupo hapa mguu kwa mguu kukagua maji haya, eneo
lililotengwa na Kiwanda kutitisha uchafu wote wa kiwanda”
Pia alisema
“Tatizo hili ni la muda mrefu, hata
mwaka jana wananchi waliandamana kwenda kwa Diwani, wakafika hadi
kiwandani, kweli baada ya hayo maandamano kiwanda kikafunga maji haya
kwa muda”
Aliendelea kueleza kuwa
“Tangu mvua zianze mwaka huu tumeona
tena maji yenye rangi ya kutisha yakitiririka kluelekea kwenye makazi
ya wananchi, mashama ya wananchi, mbaya zaidi ni kutiririkia kwenye
Mto Oloresho, kwani Mto huu wananchi wanatumia maji hayo kwa kufulia,
kuogea na Ng’ombe kunywa”
“Kinachonisikitisha kabisa nimekuwa
nikizungumza kuhusu jambo hili kwenye kikao cha maendeleo ya Kata
ambayo mwenyekiti wake ni Diwani, ila kweli Diwani hajaonyesha nia ya
dhati yakutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hili”
Hatahivyo mkt anashangazwa kuwa
“Ninashangaa zaidi kuwa viongozi wa
mtaa wa Mateves wamefumbia majo jambo hili, afisa mtendaji anatambu
ila wako kimya, wakazi wa mateves, wenye mashamba haya ambapo maji
yanakatisha na yameshakuwa kama Mto wako kimya, maji haya yanaonekana
kuwa na sumu, yanatoa harufu mbaya, kiasi cha kuchafua mazingira kwa
harufu, kutiririka bila kusahau kuhatarisha afya ya wakazi, zaidi
sana watoto ambao hawajitambui wamekuwa wkicheza kwenye mto huu wenye
maji machafu”
Balozi nae alisema
Balozi Ndugu Aminiel John ameonyesha
nae kusikitishwa na tatizo hili sugu “ndugu yangu mi ninasikitika
kwasababu eneo la Mateves ambapo kiwanda kipo na kimejenga
miundombinu mibovu ya maji taka viongozi wapo, ofisi ya mtaa ipi,
Diwani ni jirani na hapa wote wamefumbia macho ufedhuli huu”
Akizungumza kwa uchungu mwananchi John
Laizer wa Mtaa wa Mateves, alisema tulisha andika barua kwenye ofisi
ya mtaa na wilaya kueleza kuhusu shida ya kiafya inayosababishwa na
Kiwanda cha (A to Z)
“Yaani mimi nashukuru kuwaona wakazi
wenzangu wa mtaa wa Oloresho, sisi tumejaribu kupambana na tatizo
hili lakini viongozi wetu ni Bure kabisa, mwenyekiti wa mtaa hana
lolote, Diwani ndie kabisa hatutetei kabisa sisi tunaathiriwa na
Arufu mbaya ya maji taka, maji hayo yamearibu mashamba yetu, daraja
limearibika hata mtu ukitaka kutumia Gari kumpeleka mgonjwa kwa sasa
ni shida kabisa huwezi kwsababu barabara imearibiwa” alisema John
Laizer wa mtaa wa Mateves.
Wananchi Waliazimia
Wananchi walipokaa kikao tumeazimia
tukague ukweli na madhara yaliyosababishwa na maji haya, wananchi
walimeamua kwenda mguu kwa mguu kukagua maji hayo, eneo lililotengwa
na Kiwanda kutitishiwa uchafu wote wa kiwanda, hata hivyo eneo
lenyewe ni la wazi sana, ukuta umeanguka, bwawa la maji machafu
halijawekwa kulingana na Maelekezo ya Baraza la Mazingira la Taifa
(NEMC).
“Tumekagua tumejiridhisha kuwa
mwekezaji huyu ni Adui wa Mazingira, Afya na Wakazi wa Olasiti,
kwasababu kwa jinsi alivyojenga miundombinu yake ya majitaka na taka
za kiwanda ina dhihirisha kuwa alidhamiria kufanya hivi”
Azimio la Kikao na Matembezi ya
Ukaguzi wa Madhara yanayosababishwa na maji taka ya kiwandani
yatafuata baada ya kwenda kujadiliana katika kikao cha mitaa au kata
ya Olasiti kwa Ujumla kwasababu ndio wanaoathiriwa na tatizo hili,
kikao kitaamua cha kufanya.
“Na mimi ni Mwananchi wa Olasiti, mdau
wa Mazingira, Elimu na Afya, nimesikitishwa sana na Mwekezaji huyu wa
(A to Z) kutupuuza na kutudharau kiasi hiki, kimsingi ninalaani jambo
hili kwasababu ina hatarisha Uhai wa Viumbe, wanyama na binaadamu kwa
ujumla. Nasikitishwa pia na Udhaifu ulio na unao onyeshwa na Viongozi
walipewa dhamana yakuwatumikiwa wananchi wa Olasiti kutotekeleza
matakwa ya Wananchi”
Ninashauri Wananchi wa Olasiti, hasa
wa mtaa wa Mateves na Oloresho kutambua kuwa kwasasa njia pekee
iliyosalia ni kutumia “Nguvu ya Umma ili kupata Ufumbuzi wa Kudumu
wa Tatizo hili”
0 Comments