Kwa ufupi
“Serikali hutenga fedha nyingi kila mwaka kwa ajili
ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ili vijana wanaojiunga na vyuo vikuu
wakopeshwe, sasa kwa nini inaupendeleo?” alihoji.
Dodoma. Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ritta
Kabati ameihoji Serikali kuwa kwa nini Sera ya mikopo kwa elimu ya juu
inatolewa kwa kozi za sayansi na ualimu badala ya kutoa mikopo kwa kozi
zote.
“Serikali hutenga fedha nyingi kila mwaka kwa
ajili ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ili vijana wanaojiunga na vyuo
vikuu wakopeshwe, sasa kwa nini inaupendeleo?” alihoji.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Jenister Mhagama alisema utoaji wa mikopo hufuata
taratibu za kisheria na miongozo ya Serikali hasa katika vipaumbele vya
Taifa.
“Mahitaji ya kitaifa ndiyo yanayoiongoza Serikali
kuainisha programu zinazopewa kipaumbele katika kutoa mikopo kwa nia ya
kuwashawishi wanafunzi wasome,” alisema.
Alisema kuanzia mwaka wa masomo 2014/2015
vipaumbele vya Taifa ni Ualimu wa sayansi na Hisabati, Sayansi za Tiba,
Uhandisi wa umwagiliaji pamoja na gesi na mafuta.
“Sambamba na hilo, Serikali imeendelea kutoa
mikopo kwa wanafunzi wenye uhitaji wanaosoma kozi zisizo za kipaumbele
na waliokidhi viwango vinavyotakiwa katika kupata mikopo,” alisema.
0 Comments