Vodacom Tanzania wakishirikiana na Benki ya CBA, ilizindua promosheni kubwa inayojulikana kama "Jiongeze na M-Pawa" ambayo inawawezesha watumiaji wa huduma ya M-Pawa kujishindia zawadi ya fedha taslimu.
Jumla ya shilingi milioni 300 zimetengwa kwa ajili ya promosheni hiyo na mshindi mmoja wa droo kubwa atajishindia kitita cha shilingi milioni 100.
Washindi wa wiki watazawadiwa shilingi milioni 20 na washindi wa siku watazawadiwa shilingi milioni moja.
Promosheni hiyo ambayo ilianza mwanzoni mwa mwezi wa 9 itadumu kwa kipindi cha wiki sita na itafikia kilele mwishoni mwa Mwezi Oktoba, 2016.
Meneja masoko Huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania ,Noel Mazoya (katikati) akiongea na mmoja wa mshindi wa droo ya promosheni ya Jiongeza na M-Pawa wakati wa hafla ya kuchezesha droo ya pili ya wiki iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo mkazi wa Arusha Isaack Pilemon alijishindia kitita cha shilingi Milioni 20. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Meneja wa Huduma za M-Pawa wa Benki ya CBA Eric Luyangi na Msimamizi wa bodi ya michezo ya Kubahatisha nchini Bakari Maggid.
Meneja masoko Huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania ,Noel Mazoya (katikati) akiwaonyesha waandishi wa habari namba ya mshindi wa droo ya promosheni ya Jiongeza na M-Pawa wakati wa hafla ya kuchezesha droo ya pili ya wiki iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo mkazi wa Arusha Isaack Pilemon alijishindia kitita cha shilingi Milioni 20.
Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Meneja wa Huduma za M-pawa wa Benki ya CBA Eric Luyangi na Msimamizi wa bodi ya michezo ya Kubahatisha nchini Bakari Maggid. Hadi sasa washindi 2,800 wameongezea mara mbili ya akiba zao za M-Pawa washindi 14 wameshinda milioni 1 kila mmoja na washindi 2 wamejishindia milioni 20 mshindi wa jumla washilingi milioni 100 atapatikana mwezi wa kumi.
Waandishi wa habari wakifuatilia tukio la kuchezesha wa droo ya promosheni ya Jiongeza na M-Pawa wakati wa hafla ya kuchezesha droo ya pili ya wiki iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo ambapo mkazi wa Arusha Isaack Pilemon alijishindia kitita cha shilingi Milioni 20.
0 Comments