WATOTO WA MITAANI KUREJESHWA KWENYE FAMILIA ZAO

Kwa ufupi

Mushi alisema mpango huo utaendelea hadi 2022.

Dodoma. Serikali imesema kwa sasa imeandaa mpango wa miaka mitano wa kusadia watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani ili waweze kupata elimu na kuwaunganisha pamoja na familia zao.

Mushi alisema mpango huo utaendelea hadi 2022.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Kaimu Kamishina wa Ustawi wa jamii Rabikira Mushi wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya siku ya Ustawi wa Jamii ambayo yatafanyika leo kitaifa jijini Dar es salaam katika viwanja vya ustawi wa jamii Kijitonyama.

Alisema serikali imeandaa mpango wa miaka mitano ambao utasaidia idara hiyo ya ustawi wa jamii kuwafikia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kufanya kazi mitaani ili waweze kupata elimu kama ilivyo kwa watoto wengine.

 

0 Comments