Ofisa wa Benki ya NMB kushoto akimkabidhi kadi yake ya benki mshindi wa shindano la bahati nasibu ya Biko baada ya kushinda Sh Milioni 10 za shindano hilo nchini Tanzania. Anayeshuhudia kulia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven. Makabidhiano hayo ya fedha na kadi ya benki kwa mshindi huyo yalifanyika Makao Makuu ya benki ya NMB kama sehemu ya kumuandaa mshindi wa Biko kuzitumia fedha zake kwa uangalifu ili zimnufaishe kiuchumi.
MSHINDI wa shindano la bahati nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, Christopher Mgaya, jana amepokea fedha zake sambamba na kupewa elimu ya kifedha kutoka Benki ya NMB ambapo alifunguliwa akaunti ya kuhifadhia fedha hizo.
Mgaya alitangazwa mwishoni mwa wiki katika droo ya kwanza ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10, droo iliyochezeshwa na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja akishirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Juhudi Ngolo, jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa Sh Milioni 10 wa mchezo wa kubahatisha wa Biko, Christopher
Mgaya, akisikiliza wakati Meneja Masoko wa Biko Tanzania, wachezeshaji wa bahati nasibu ya Ijue Nguvu ya Buku, Goodhope Heaven, wakati anafanya mazungumzo na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam. Fedha hizo alikabidhiwa jana Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam sambamba na kupewa elimu ya kifedha ili fedha hizo zimnufaishe kiuchumi na kubadilisha maisha yake.
Nia ya kufunguliwa akaunti katika tawi la NMB Makao Makuu jijini Dar es Salaam sambamba na kupatiwa elimu ya kifedha kwa mshindi huyo limetokana na kiu ya kumuandaa kijana huyo ili aweze kuzitumia ipasavyo fedha zake kwa ajili ya kumuinua kiuchumi kutokana na uwapo wa mchezo wa bahati nasibu huo unaochezwa kwa kufanya miamala ya kifedha kwenye Tigo Pesa, Mpesa na Airtel Money.
Mshindi wa Sh Milioni 10 wa mchezo wa kubahatisha wa Biko, Christopher Mgaya, akipokea fedha zake alizoshinda baada ya kutangazwa mwishoni mwa wiki na kukabidhiwa mapema jana Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam sambamba na kupewa elimu ya kifedha ili fedha hizo zimnufaishe kiuchumi na kubadilisha maisha yake. Kulia kwake ni Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven.
0 Comments