TAFAKURI YA MWALIMU

Kwa mchoro huu;
Ninajaribu kufikiri kuhusu #Elimu ikiwa bajeti ya 2017/18 ndio itamalizia viporo basi tutakuwa na hali ngumu sana kwenye Ubora na Utoaji wa Elimu hasa kwa shule za serikali.

Kuna shule ambazo zinadaiwa ma milioni kutokana na Huduma mbalimbali za wazabuni waliozihudumia shule husika mfano; chakula, vifaa vya maabara, vitabu na Stationeries basi maendeleo ya Elimu nadhani yataingia kwenye mkwamo mkubwa wa kulipa madeni badala ya kujenga uwezo kwa walimu, kujenga nyumba za walimu, kujenga miundombinu rafiki kwa wanafunzi kujifunzia na kuongeza vifaa ambavyo havipo shuleni.

Labda wazabuni wote warushwe/ wasilipwe madeni ili kitakachoelekezwa kwenye #Elimu ikaboreshe ubora wa #Elimu, ila katika sifa za utawala bora kutolipa deni la wazabuni ni sahihi?

Hivyo basi nadhani wadau wahusishwe zaidi kuboresha Elimu yetu, ni kweli serikali inagharamia elimu kwa sasa ila naona itazidiwa kwani sekta hii inamahitaji mengi na mengine huwenda yasiishe kutatuliwa.

Ni vema wazazi, wadau mbalimbali kuendelea kuhamasishwa kuchangia na kushiriki uboreshaji wa #Ubora wa #Elimu yetu bila kusubiri bajeti pekee.

Elimu Afrika

0 Comments