Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Temeke, Eric Kilangwa (wa pili kulia) na Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick wakifurahia baada ya uzinduzi wa madarasa matano, ofisi ya walimu na eneo la makusanyiko baada ya kufanya ukarabati katika shule ya sekondari Barabara ya Mwinyi iliyopo Buza jijini Dar es Salaam Juni 6 2017. Pamoja nao ni Mwenyekiti wa shule hiyo, Sostenes Nyenyembe (kulia), Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Bam International Africa Noreen Mazalla (kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Emmentrudice Chilewa.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Emmentrudice Chilewa akiwatembeza wageni kujionea ukamilishwaji wa mradi wa ukarabati wa madarasa na ujenzi wa eneo la makusanyiko kabla ya kufanya uzinduzi.
Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Barabara ya Mwinyi alipotembelea mojawapo ya madarasa matano, kampuni hiyo iliyoyakarabati eneo la Buza jijini Dar es Salaam Juni 6 2017. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Emmentrudice Chilewa.
Waalimu na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bam International wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Barabara ya Mwinyi iliyopo Buza jijini Dar es Salaam wakati wa hafla hiyo.
0 Comments