Leo tarehe 7/6/2017 Prof. Deus Ngaruko Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania atazungumza mubashara katika Televisheni ya CHANNEL TEN kuanzia saa 4 kamili usiku. Lengo kuu la kipindi hicho ni kuwaalika Wananchi wote wenye sifa za kujiunga na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kuomba nafasi mbalimbali za masomo kwa mwaka wa masomo wa 2017/2018.
Hii itakuwa ni fursa nzuri kwa Watanzania na wasio wa Tanzania kufahamu kwa mara nyingine tena fursa za masomo zinazotolewa na chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
0 Comments