TUSOME VITABU

Kwa katuni hii;
Hali halisi katika rika mbalimbali nchini wanajamii wamejikita na kuamini mitandao ya jamii kuliko vitabu vya mashwala mbalimbali.

Nabashiri huku tuendako maktaba itakuwa ya kuhifadhi vitu vya kale badala ya kuwa chimbuko la maarifa, taaluma, na elimu kwa ujumla wake.

Wito wetu kwa wanafunzi, vijana na wazazi kusisitiza usomaji wa vitabu badala ya "USO wa Kitabu" Facebook, tafsiri sio rasmi. Kimsingi jamii inaelekea kusubiri kilichoandikwa na watu kwenye mitandao badala ya kupata uhakika wa maswala kadha wa kadha toka kwa wataalamu husika au vitabu husika vya mambo.

Tusome vitabu, tujisomee

Elimu Afrika
"Jitahidi kujielimisha kwa kadri ya uwezo wako na kutumia elimu hiyo kwa faida ya wote"

Tufuatilie kupitia, Instagram: @elimuafrika, Facebook: Elimu Afrika, Twitter: @ElimuAfrika na YouTube: Elimu Afrika na www.elimuafrikatz.blogspot.com #SiasaIsiingilieTaaluma.

0 Comments