Elimu Afrika inaunga mkono jitihada za Mbunge wa Afrika Mashariki Shyrose Banji la kuhamasisha Elimu ya kuhusu Jumuia ya Afrika Mashariki kufundishwa kwenye shule zote za msingi na sekondari katika nchi zote sita za Jumuia.
Napenda ifahamike kuwa Tanzania shule za msingi na sekondari zinafundisha kuhusu Jumuia kwenye masomo ya Uraia/Civics na Historia/History, na kidato cha tano na sita/ A-level hufundishwa kwenye somo la General Studies na Jografia/Geography hivyo kupeleka Elimu hii kwa nchi wanachama ni jambo la muhimu na lamsingi sana.
Ni vema Elimu hii isijikite kwenye mfumo rasmi wa elimu tu, bali utumike kwenye mifumo yote mitatu ya mifumo, ambayo ni; (a) Mfumo rasmi (b) Mfumo Uliondani ya Rasmi (c) Mfumo Usiorasmi.
Ni ahadi yetu kusisitiza wanafunzi wote Afrika Mashariki kujitahidi kujielimisha kwa kadri ya uwezo wao na kutumia elimu hiyo kwa faida ya wote.
Tufuatilie kupitia, Instagram: @elimuafrika, Facebook: Elimu Afrika, Twitter: @ElimuAfrika na YouTube: Elimu Afrika.
#SiasaIsiingilieTaaluma.
0 Comments