Ndugu zangu,
Mwandishi na mwanafalsafa Mtanzania, Shaaban Robert aliishi mbele ya wakati wake.
Kupitia maandiko yake, Shabaan Robert aliweza kuzisawili desturi za Wasadikika.
Kama alivyopata kusema; kuwa Wasadikika kwa desturi ni watu wenye kupuuzia mambo mpaka pale yanapowaletea madhara.
Ni hivyo, hata leo, tumekuwa ni watu wa kutanguliza mizaha hata kwenye mambo ya msingi.
Ona kibao hicho cha mtaa, wenye kuhusika wametulia tu wakati aliyeandikwa kwenye mtaa huyo hajapata kuwepo kwenye Nchi Ya Kusadikika, eti Shabaani Robert badala ya Shabaan Robert!
Na ikitokea ukakutana na muhusika kumuuliza ilikuwaje wakafanya kosa hilo, naye atajikung'uta kama jogoo aliyenyeshewa na mvua na kukuuliza;
" E bwana ee, kwani huyo jamaa una undugu naye?!"
Naam, Nchi Ya Kusadikika haijapata kukumbwa na ukame wa maajabu.
Maggid.
0 Comments