WAHITIMU 26 WA VSOMO WAKABIDHIWA VYETI, DAR


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya, akizungumza wakati wa kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya VSOMO, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Veta Kipawa, Sospeter Mkasanga.

Mkuu wa Chuo cha Veta Kipawa, Sospeter Mkasanga, akizungumza wakati wa kukabidhi Vyeti kwa Wahitimu wa Mafunzo ya VSOMO kupitia Mtandao wa simu wa Kampuni ya Airtel Tanzania.Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya.

Mkuu wa Chuo cha Veta Kipawa, Sospeter Mkasanga, akimkabidhi cheti mhitimu wa Mafunzo ya VSOMO kupiti mtandao wa Simu wa Airtel Tanzania, Elias Joseph. Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya.

Mkuu wa Chuo cha Veta Kipawa, Sospeter Mkasanga,akimkabidhi cheti mhitimu wa Mafunzo ya VSOMO kupiti mtandao wa Simu wa Airtel Tanzania, Mohammed Ali Mohammed.Katikati ni ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya.

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) leo imekabidhi vyeti kwa wanafunzi26 waliohitimu mafunzo ya ufundi stadi kwa njia ya mtandao kupitia aplikesheni ya VSOMO ambapo kati yao wanafunzi 18 ni kutoka VETA kipawa na 8 VETA Mwanza

VSOMO ni mfumo unaotoa mafunzo ya ufundi stadi kwa njia ya mtandao unaotolewa chini ya ushirikiano kati ya kampuni ya simu ya Airtel pamoja na Mamlaka ya mafunzo stadi VETA ambao unalenga kuleta tija katika mapinduzi ya elimu nchini.

Akiongea wakati wa kukabidhi vyeti, Mkuu wa VETA Kipawa, Bwn Sospeter Dickson Mkasanga aliwapongeza Airtel kwa kushirikiana nao katika kuanzisha aplikesheni ya VSOMO inayowawezesha wanafunzi kupata masomo ya ufundi wakati wowote mahali popote nchini kupitia simu zao za mkononi. Pia aliwapongeza wanafunzi waliamua kutumia technologia ya simu katika mambo ya msingi na kupata vyeti”.

Mkasanga aliongeza kwa kusema lengo kubwa la kutumia mfumo huu wa njia ya mtandao ni kuongeza wigo wa upatikanaji wa mafunzo ya ufundi katika maeneo mbalimbali nchini, jitihada zinazoenda sambamba na adhima ya Serikali ya kutoa elimu kwa wote hususani watanzania waishio katika maeneo ya pembezoni mwa nchi. tumeanza kuona jinsi mfumo huu umeanza kuleta tija ambapo mpaka sasa wanafunzi 105 wameshahitimu mafunzo yao na kati ya 36 wanafanya mafunzo ya vitendo katika vituo mbalimbali vya VETA nchini. Hii kwetu ni hatua kubwa kuelekea kuwawezesha watanzania wote kufikiwa na masomo ya ufundi ili kuwa na nguvu kazi yenye ueledi. Napenda kuwapongeza vijana wanahitimu masomo yao leo na kuwahamasisha jamii kuendelea kujiandikisha katika masomo haya”.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrce Singano Mallya “ tunajivunia kushuhudia mabadiliko katika matumizi ya technologia ya simu kwa kuwezesha maelfu ya watanzania kusoma kupitia simu zao za mkononi. Lengo letu ni kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi kwa kuwatengenezea program mbalimbali zitakazowasaidia kukuza ujuzi na kuleta ufanisi katika shughuli za kijamii na kiuchumi. Tunaamini VSOMO utawavutia vijana wengi kujiunga na masomo ya ufundi kwani inaenda sambamba na ukuaji wa technologia, ni ya gharama nafuu na rahisi kupatikana kupitia simu zao za mkononi lakini pia masomo yake yamedhibitishwa na mamlaka ya ufundi stadi VETA”.

“tunapenda kuendelea kuwahakikishia kuwa Airtel itaendelea kushirikiana na VETA pamoja na mashirika mengine katika kuhakikisha inatumia techonologia ya simu kutatua changamoto na kuchangia katika kukua kwa uchumi wa nchi kwa ujumla” aliongeza Mallya

Kozi 13 za ufundi zinapatikana katika aplikesheni ya VSOMO ni pamoja na Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo ya kompyuta, umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani, Umeme wa magari. Vilevile Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi wa simu za mkononi, Ufundi Alluminium, Utaalamu wa maswala ya urembo pamoja ma Ufundi wa kuchomea vyuma.

0 Comments