MWANZFUNZI ANTHONY PETRO APATA UFADHILI WAKIMASOMO.

Safari ya mtoto Anthony Petro mkazi wa Ngara mkoani Kagera kwenda masomoni katika Shule ya Amani Humwe wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro, imeanza leo Jumapili Aprili 8, 2018.
Akiwa mwenye uso wa furaha, Anthony (10) amesema anakwenda kutimiza ndoto ya kusaidia familia yake atakapopata kazi.
Anthony ameahidi kufanya vizuri darasani akisisitiza baba na dada zake wawili wahamishwe ili waishi sehemu yenye usalama. 
"Sijui Kiingereza nikienda shule watanifundisha niwe naongea kama Wazungu," amesema Anthony.
Mtoto huyo anapelekwa shule na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Ngara, Aidan Bahama akifuatana na ofisa ustawi wa jamii, Mussa Balagondoza.
Bahama amesema Anthony kesho atakabidhiwa kwa mfadhili wake, Isihaka Msuya ambaye ameahidi kugharimia kila kinachohitajika kitaaluma.
Amesema halmashauri itafuatilia kila hatua ya masomo yake na likizo za kila muhula.
Ufadhili kwa Anthony na ndugu zake, unatokana na mtoto huyo kuzuia baba yake kuuza shamba.

0 Comments