SERIKALI inatarajia kuajiri walimu 6,000.
Walimu watakaoajiriwa ni wa masomo ya hisabati na sayansi kwa ajili ya shule za sekondari ifikapo Juni 30, mwaka huu.
Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Joseph Kakunda alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali aliyetaka kujua mikakati ya serikali katika kuondoa changamoto katika shule za kata ikiwamo upungufu wa walimu wa hisabati na sayansi. Amesema hadi Desemba mwaka 2017, Serikali ilikuwa imeajiri walimu 200 wa Hisabati na Sayansi kwa ajili ya shule za sekondari.
Aidha, Kakunda amesema serikali haijazuia wananchi kuchangia maendeleo ya shule walichokataza ni kumzuia kumpa adha ya kukosa masomo mwanafunzi ambaye ameshindwa kuchangia michango hiyo. Katika swali la pili la nyongeza, Bobali alitaka kujua msimamo wa serikali kuhusu wananchi kuchangia kwenye chakula ambacho wameona kuwa ndiyo mwarobaini wa ufaulu kwa wanafunzi katika Mkoa wa Lindi. Katika swali la msingi la Bobali alitaka kujua kama serikali imefanya tathmini juu ya ubora na changamoto zilizopo katika shule za sekondari za kata nchini.
0 Comments